Saturday, August 29, 2015

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Wakati mshambulizi Mrundi, Kelvin Ndayesenga akitaraji kurudi nchini kukamilisha usajili wake wa kujiunga na Simba SC, Betram Mwombeki ambaye ni mshambulizi-pacha wa zamani wa Amissi Tambwe katika timu hiyo ya ‘  Mitaa ya Msimbazi’ katikati ya jiji la Dar es Salaam amefunguka na kusema ni hadi pale viongozi/wahusika wa usajili katika timu hiyo watakapoacha ‘ ubinafsi’ na kutengeneza mifumo mizuri ya kiutawala ndipo wanaweza kupata mafanikio.
Akizungumza na mwandishi wa www.shaffihdauda.co.tz ( Baraka Mbolembole) mapema Jumamosi hii akiwa jijini Mwanza, Betram ambaye amepumzika kucheza mpira wa ushindani baada ya kucheza nchi za Uganda, Rwanda, Kenya alisajiliwa na Simba katikati ya mwaka 2013 akitokea nchini Marekani alidumu kwa msimu mmoja tu katika timu hiyo licha ya kufanya vizuri sambamba na Tambwe katika safu ya mashambulizi.
Hivi navyoandika ni kwamba washambuliaji wote wawiwli, Betram na Tambwe hawapo katika timu hiyo na klabu imekuwa ikitumia pesa nyingi kupata wafungaji. Mwombeki amekosoa mfumo mzima wa kimpira, kiutawala huku akisimulia baadhi ya matukio yasiyo vutia aliyowahi kukutana nayo ndani ya klabu ya Simba.
Haya hapa mahojiano yangu na Betram……
www.shaffihdauda.co.tz; Umecheza Simba kwa muda mfupi lakini ulifanya vyema, nini sababu inayokufanya upumzike mpira kwa sasa?
Betram Mwombeki; Sijapumzika kucheza mpira kila siku nacheza na nisipo cheza basi nitafanya ‘matizi’ yoyote ya kuhusiana na shughuli hiyo , pia kwa sasa nina shughuli zangu nyingine zinaendelea kama kawaida. Lingine siyo kama niliachwa Simba ndiyo ‘ nakakasirika’ mpaka ifikie hatua ya kuuchukia mpira au kuacha lakini mimi nachukia sana ‘system’ yetu ya mpira wa kibongo kulinganisha na sehemu zingine nilipokuepo nacheza. 
www.shaffihdauda.co.tz;  Mfano, ni yapi hayapo sawa katika mfumo wetu wa mpira?
Betram Mwombeki’; Mimi ni  ‘mkubwa’ naongea kutoka moyoni na ukweli ‘ najua watu hawapendi ukweli ukiongelewa’ na wanakuchukia lakini mie  ‘ I don't care’  kwani siku ya mwisho ukweli utatakiwa uongelewe ili tuweze kujenga na kutatua ambacho kinasumbua
Naweza nikasema kwamba mfumo wetu wa bongo umekuepo kama siasa ambayo ‘ imeingia uchafu ndani yake’ na ‘wadadu’ au wana ongoza soka letu la bongo wengi wao siyo watu ‘ waliolifuzu’ kwenye hiki kitu au hawakuwahi kucheza kuona ni nini wapaswa kufanya. 
www.shaffihdauda.co.tz; Ulipotoka Marekani na kujiunga Simba siku ya kwanza ulipofika mazoezini uligundua tofauti gani kati ya maisha ya kimpira huko ulipokuwa na ile ya Simba?
Betram Mwombeki; Hahahahahaha siku ya kwanza sikuona kitu lakini tulivyo anza kusafiri kwenda mikoani kucheza’ friendly games’ hapo kabla hatujasajiliwa kuna kitu nilikiona nikasema hapa hamna kitu hii ni ‘miyeyusho mitupu’ ,  kwani timu ilikuwa inasafili kama timu ya ‘ ndondo’  bila camera man bila management yeyote bila jezi ya timu ili tuweze ‘ kuadivatazi’  timu yetu yaaani vitu vingi sana kiasi kwamba nikaona ni kitu cha kienyeji sana,  tulivyo fika Tabora nilikataa kulala kitanda kimoja na mchezaji mwenzangu yaaani noma na ‘ Rage akasema wewe Mmarekani sana hapa Bongo’
Betram Mwombeki; Hilo si kwenye timu tu,  pia kwa hii ni system ya maisha ya bongo tunakopi na kupesti  ‘mimi nikiwa kocha wa timu hapa bongo definitely ntaleta watu wangu na ntachukia watu wallio letwa na viongozi wengine bila sababu hata kama kazi wanaweza’
Kwenye Shirikisho la mpira la kibongo ni kama chama cha siasa yaani kama mimi nikipata namleta na mdogo wangu na mdogo angu anamleta anaemfuata ili tupige pesa sio kazi 
www.shaffihdauda.co.tz; Ulipewa fomu na kusaini baada ya siku ngapi tangu uliojiunga kwa majaribio chini ya walimu, King na Julio?.
Betram Mwombeki; Hahahaha kwanza walikuwa  wanataka nisaini bure ‘ eti kwa sababu walikuwa’  wananiona leo nakuja na Range kesho Benz aaah huyu  wakawa wanasema ‘ Mmarekani hataki pesa na hata haitaji pesa zenu mtakazo mpa’ .
Wakaanza kunipotezea muda kila wakati watu wangu walipokuwa wanaongea nao mpaka nakumbuka kuna mechi moja tulikuwa tunaenda kucheza Tanga na Coastal usiku wake watu wangu wakaja Bamba Beach kule camp na kuwaambia ‘ huyu aendi Tanga mpaka kila kitu kiwe tayari hapa’.
 Zilikuepo zimebakia siku kadhaa tu kabla ya kufuingwa kwa usajili  na nilikuwa niende Azam lakini Azam walikuwa  wamemaliza usajili na wanakwenda South basi walivyo rudi wakasikia naenda Yanga hapo ndiyo Simba wakastuka na kukamilisha mapema
www.shaffihdauda.co.tz; Nini kilitokea?
Betram Mwombeki; Basi tu walikuwa wanataka nisaini bure lakini Namshukuru Mwenyezi Mungu nilipata nilichokipata na lengo langu kubwa ni kucheza nyumbani kwani nilikuwa nimecheza Uganda Rwanda na Kenya kidogo lakini sikukamilisha malengo yangu sasa nikaona hapa itakuwa fresh , kwanza ni home.
www.shaffihdauda.co.tz; Ulifanya vizuri ulipocheza na Amis Tambwe miaka miwili iliyopita. Kwanini wote hamko Simba SC kwa sababu?
Betram Mwombeki; Kwanza  naweza kusema  timu zetu kubwa siyo za kujenga wachezaji au kutengeneza wachezaji au kujua nani anafa kucheza na nani kwani mwisho wa siku Kibadeni alikuwa  hapewi mamlaka yote ya timu na kufanya uamuzi wa mwisho kwa hilo labda mimi nilikuwa nafaa kucheza na Tambwe au na mtu mwingine tofauti na Tambwe lakini they didn't c that na pia Tambwe ni mchezaji ambaye anahitaji mtu wa ‘ kuchafua harafu yeye anafagia’.
Nirudi kwenye shwali lako tuliondoka wote kwa sababu ya system mbovu iliyokuwa inaendeshwa pale na kulikuepo kuna uongozi mwingine nje ya ule wa kikatiba, waliokuwa madarakani then walikuwepo wanaotaka kuingia madarakani so wakachafua ili nao wapate yaaani ‘ usida juu ya usida’
www.shaffihdauda.co.tz; Ungekuwa kiongozi wa Simba ungefanya nini ili klabu iwe na timu bora ya muda mrefu?. Tunaizungumzia zaidi Simba kwa sababu ni klabu kubwa ya michezo Tanzania pia umewahi kuajiriwa pale kama mchezaji.
Betram Mwombeki; Duh kazi ngumu sana hiyo lakini cha kwanza nisingelikubali timu iwe ya wanachama na kuruhusu matajili wawekeze kwenye timu hapo tungepata uwezo wa kupata Academy ya muda mrefu ili tuweze kukuza vipaji vya hapa kwanza kwani mimi sioni ‘ solution’  ya kukosa wachezaji hapa na kwenda kuchukua sehemu nyingine .
Mwisho kupitia pesa tutakazo zipata tuta invest kwene mambo mengine beside mpira kama vile kujenga hotels kila mkoa kununua mabasi ya biashara kujiingiza kwenye kilimo na ufugaji kujenga mashule na tunaanza hapa na kuxpandi pole pole kwenda kimataifa pia na shughuli zote hizo ziitwe Simba au ziusishe na jina hilo ili tupaishe timu yetu ijulikane duniani kote..!!
Itaendelea……0714 08 43 08

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video