Hatimaye Bayern Munich wameibuka mabingwa wa Audi Cup ikiwa ni kombe la maandalizi ya msimu mpya.
Bayern jana usiku wameichapa 1-0 Real Madrid katika mechi ya fainali iliyopigwa uwanja wa Allianz Arena, Mjini Munich, Ujerumani.
Bao pekee la Bayern inayonolewa na Pep Guardiola lilifungwa na Robert Lewandowski dakika ya 87.
Hata hivyo katika mechi hiyo ya jana, kulitokea kituko cha ambapo Toni Kroos alitolewa na kocha wake Rafa Benitez na nafasi yake kuchukuliwa na Danilo.
Wakati Kroos akienda kukaa benchi, Gareth Bale alinyoosha mkono akitaka kumsalimia ikiwa ni ishara ya kumsapoti kwa kazi aliyofanya (tazama picha chini)
Kwa bahati mbaya Kroos hakumuona Bale na watu wakaanza kuhisi wawili hao wana msuguano.
Baadaye wakiwa kwenye ndege kurejea Madrid, Hispania, Bale ali-post picha ikimpa tano Kroos kuashiria kwamba hawana tatizo lolote na wamesameheana kwa kilichotokea.
Tazama picha chini:
Hata hivyo,Cristaino Ronaldo na Gareth Bale hawakucheza mechi hiyo.
0 comments:
Post a Comment