Wakati Yanga wakienda kujificha Mbeya kwaajili ya maandalizi ya ligi kuu na mechi ya ngao ya jamii, mabingwa wa Kombe la Afrika Mashariki “Kagame Cup”, Azam FC wanaondoka leo asubuhi kuelekea Kisiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi zaidi.
Azam FC inaingia msituni kujiwinda na mechi yao ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga itakayochezwa mwishoni mwezi huu kabla ya kuanza kwa mikikimikiki ya Ligi Kuu Bara.
Kocha mkuu wa kikosi hicho, Stewart Hall aliwapa mapumziko wachezaji wake mara tu baada ya kuchukua ubingwa huo uliowafanya waandike historia mpya kwani ni mara ya kwanza kutwaa Kombe hilo pia walicheza bila kuruhusu bao hata moja langoni mwao.
Azam itacheza na Yanga mechi hiyo baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi na Yanga ikiwa ni mabingwa.
0 comments:
Post a Comment