Winga mpya wa PSG aliyesajiliwa kutoka Manchester United, kwa dau la paundi milioni 44, Muargentina, Angel di Maria jana aliitazama timu yake akiwa jukwaani na bahati nzuri ikashinda 1-0 dhidi ya Lille katika mechi ya ufunguzi wa ligi kuu nchini Ufaransa, League 1.
Bao pekee la ushindi la PSG lilifungwa kipindi cha pili na Mbrazil, Lucas Moura.
Hata hivyo PSG walimaliza mechi hiyo ya ugenini wakiwa pungufu kufuatia Adrien Rabiot kuoneshwa kadi nyekundu kutokana na kumvuta jezi mpinzani wake.
0 comments:
Post a Comment