Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu leo amezindua michuano ya Airtel Rising Star kwa mkoa wa Dare salaam, ambapo timu kutoka wilaya za Ilala, Temeke na Kinondoni zinashikriki michuano hiyo.
Akifungua michuano hiyo, Zungu amewatikia vijana kutumia vizuri nafasi hiyo ya michuano ya Airtel Rising kuonekana, kwani kutawapelekea kupata nafasi ya kucheza katika timu kubwa na kuweza kuendesha maisha yao kwa kupitia mpira wa miguu.
Michuano ya Airtel Rising Stars imekua ikifanyika kila mwaka nchini kwa lengo la kusaka na kuibuka vipaji vya wachezaji wenye umri chini ya miaka 17, ambapo wachezaji wenye vipaji huchaguliwa na kupelekwa katika vituo vya kufundisha soka na wengine huchaguliwa katika kikosi cha Taifa cha Vijana (Serengeti U17).
0 comments:
Post a Comment