Mshambuliaji
msumbufu na mwenye majivuno, Zlatan Ibrahimovic maarufu kama 'Cadabra' amesema
angependa kuichezea Manchester United siku moja lakini anahofia 'ngumi' za kila
siku na kocha Louis Van Gaal.
Akiwajibu
waandishi wa habari kama yuko tayari kujiunga na mashetani hao wekundu, Cadabra
alisema angeweza kuchezea United lakini anahofia ugomvi wa kutoisha baina yake
na Louis Van Gaal.
Zlatan na
Van Gaal hawakuwa na mahusiano mazuri tangu wakiwa Ajax miaka ya 1990's lakini
moto uliwaka zaidi baada ya Zlatan kumtaja Van Gaal kama 'pampasi' katika kitabu
chake.
Wawili hao
hawana urafiki na kwamba hawawezi kuiva chungu kimoja. Hisia zimekuwa ni nyingi
miongoni mwa mashabiki mara baada ya kocha Louis Van Gaal kutangaza kwamba atafanya
usajili wa kushitukiza wa mshambuliaji siku za usoni.
Hata hivyo Cadabra
nahodha wa Sweden anahusishwa na tetesi za kujiunga na AC Milan ya nchini Italia.
Habari zinasema Zlatan amechoshwa na quality ya ligi nchini Ufaransa na sasa
anafikiria kuihama klabu yake ya Paris St. Germain.
0 comments:
Post a Comment