Wednesday, July 29, 2015

Leo zinapigwa robo fainali za pili za michuano ya Kagame CECAFA Cup, mechi ambayo inapewa uzito wa juu ni kati ya Yanga na Azam FC ambapo wengi wanasema hii ni mechi ya fainali hata kabla ya kuchezwa kwa fainali yenyewe. Kwa hivi karibuni timu hizi zimekuwa na upinzani wa hali ya juu kutokana na ubora wa vikosi vyao pamoja na walimu wanaozinoa timu hizo.
Hapa tunaangalia mambo kadha wa kadha yanaoifanya mechi hiyo kutabiriwa kuwa kuwa ni fainali kabla ya fainali yenyewe kufika.
Historia ya timu hizi kukutana kwenye Kagame:
Yanga na Azam zilikutana kwenye michuano hii kwa mara ya mwisho kwenye hatua ya fainali mwaka 2012. Magoli kutoka kwa Hamis Kiiza na Said Bahanuzi yakaipa Yanga ubingwa wa kombe la Kagame mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza na  ya mwisho kwa Azam kutinga kwenye hatua ya fainali ya michuano ya Kagame wakati kwa upande wa Yanga wao ilikuwa ndio mara ya mwisho kutwaa taji la Kagame kwa jinsi historia inavyoonesha.
Yanga na Azam zilivyofuzu kutoka kwenye makundi kuingia robo fainali:
Azam na APR ndio timu pekee ambazo zilimaliza zikiwa hazijapoteza hata mchezo mmoja kwenye makundi yao. Azam imefuzu kutoka kundi C ikiwa na pointi tisa baada ya kushinda michezo yote na haijaruhusu goli hata moja kwenye mechi zake tatu. Imefunga jumla ya magoli tisa mpaka sasa, ilianza kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya KCCA, ikaifunga Malakia 3-0 kwenye mchezo wa pili na kumaliza kwa dozi kali ilipokutana na Adama Ciy kwa kuitandika goli 5-0.
Yanga ilinza kwa kupewa kichapo cha goli 2-1 kutoka kwa Gor Mahia kwenye mchezo wao wa ufunguzi, baadae wakashinda kwa oli 3-0 mbele ya Teleco kabla ya kushinda mchezo wao mwingine kwa goli 2-0 dhidi ya KMKM na kumaliza kwa ushindi wa goli 1-0 na kumaliza ikiwa nafasi ya pili kwenye kundi A nyuma ya Gor Mahia.
Mechi zao za mwisho kwenye makundi (Kagame Cup 2015):
Azam ilishinda kwa goli 5-0 kwenye mechi yake ya mwisho ilipocheza na Adama City huku ikionekana kucheza soka safi na la kuvutia. Kwenye mchezo huo kocha wa Azam Stewart Hall aliwaweka benchi wachezaji wake wengi kama Shomari Kapombe, John Bocco, Didier Kavumbagu, Frank Domayo na Aishi Manula.
Kwa upande wa Yanga, mechi yao ya mwisho kwenye kundi A walikutana na Al Khartoum ya Sudan na kufanikiwa kushinda kwa goli 1-0. Kama ilivyo kwa Azam, Yanga nao waliwapumzisha nyota wao wengi kwenye mchezo huo. Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Donald Ngoma, Mwinyi Hajji pamoja na Juma Abdul walianzia kwenye benchi.
Wachezaji wa kuchungwa kwenye timu zote mbili:
Kwa upande wa Yanga, wachezaji hatari ni pamoja na Donald Ngoma ambae ana goli moja kwenye michuano hii, licha ya kupata kadi nyekundu kwenye mechi ya ufunguzi mchezaji huyu ameonekana kuwasumbua sana mabeki wa timu pinzani. Ananguvu, anaweza kukaa na pira na pia aweza kucheza mipira ya juu.
Kwa Azam wao wachezaji wakuangaliwa sana ni John Bocco ambae ameonekana kurudi kwenye ubora wake kupitia micuano hii, Frank Domayo na Jean Mugiraneza ni wachezaji wengine ambao wamefanya vizui kwenye eneo la katikati hasa ukizingatia leo Salum Abubakar atakosekana kutokna na kuwa majeruhi.
Pascal Wawa hakuna asiyejua ugumu wa kumpita beki huyu na leo atakuwa akiongoza safu ya ulinzi kwa kushirikiana na Agrey Morris Shomari Kapombe na Erasto Nyoni au Michael Gadiel. Kipre Tchetche ni mchezaji ambae anaweza kufanya kitu chochote uwanjani na kubadilisha matokeo
Mfumo unaotumiwa na timu hizi:
Kocha wa Azam Stewart Hall anatumia walinzi wanne, viungo watano na mshambuliaji mmoja (4-5-1) wakati kocha wa Yanga Hans van Pluijm anatumia walinzi wanne, viungo wanne na washambuliaji wawili (4-4-2). Kitu wanachojivunia Yanga ni uwezo wao wa kucheza mipira mirefu kutokana na wachezaji wake kuwa na uwezo wa kukimbia, Simon Msuva japo hajafanya vizuri kwenye michuano hii lakini ni mchezaji mwenye uwezo wa kukimbia mtu kama Mwashiuya na Kaseke wote wanaweza kukimbia.
Azam wao silaha yao kubwa tangu kuanza kwa mashindano haya ni mchezo wao wa pasi nyingi na hii inatokana na kuwa na wachezaji watano katika eneo lao la katikati.
Wachezaji ambao wameshawahi kucheza kwenye timu zote mbili:
Azam wanawachezaji ambao tayari walishacheza Yanga kabla ya kuijiunga na ‘wanalambalamba’, Frank Domayo na Didier Kavumbagu ni wachezaji wa Azam ambao wameshawahi kukipiga Yanga. Kabla ya Domayo na Kavumbagu, Azam walishamsajili Mrisho Ngassa kutokea Yanga lakini Yanga wao walimchukua Simon Msuva kutoka kikosi cha vijana cha Azam.
Matokeo ya mechi zilizozikutanisha Azam na Yanga:
Mei 6, 2015
Yanga 1-2 Azam
Desemba 28, 2014
Azam 2-2 Yanga
Machi 19, 2014;
Yanga 1-1 Azam
Septemba 22, 2013;
Azam 3-2 Yanga
Februari 23, 2013;
Yanga 1-0 Azam
Novemba 4, 2012;
Azam 0-2 Yanga
Machi 10, 2012;
Yanga 1-3 Azam
Septemba 18, 2011;
Azam 1-0 Yanga
Machi 30, 2011;
Yanga 2-1 Azam
Oktoba 24, 2010;
Azam 0-0 Yanga
Machi 7, 2010;
Yanga 2-1 Azam
Oktoba 17, 2009;
Azam 1-1 Yanga
Aprili 8, 2009;
Yanga 2-3 Azam
Oktoba 15, 2008;
Azam 1-3 Yanga

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video