Baada ya kuwepo na taarifa kwamba, kiungo hodari wa Yanga na nahodha wa timu ya taifa ya Ruanda Haruna Niyonzima kwamba ameitoroka klabu hiyo kufuatia kutoonekana kwa muda mrefu kwenye mazoezi ya mabingwa hao wa ligi kuu Tanzania bara japokuwa likizo kwa wachezaji imekwisha na wachezaji wote wameshariboti na kujiunga na timu. Yanga imelitolea ufafanuzi jambo hilo.
Yanga kupitia kwa katibu wake mkuu Dkt. Jonas Tiboroha imekanusha uvumi huo na kusema kuwa, mchezaji huyo hajaitoroka klabu yao na wanataarifa za kuchelewa kwake kuijunga na kikosi chao ambacho tayari kimeanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Kagame pamoja ligi kuu msimu ujao.
“Wiki iliyopita Niyonzima alifiwa na mdogoake, mdogoake alikua amekwenda kuogelea ‘somewhere’ bahati mbaya akafariki kwahiyo taarifa tulikuwa tunazo kwamba amefiwa na alikuwa na msib”, amesema Tiboroha.
“Sasa kwa bahati mbaya sana juzi pia wakati yupo kwenye mipango ya kurudi huku, watotowake mapacha ambao wamezaliwa miezi michache iliyopita wakashindwa kutoka ndani ya Ruanda kuja huku (Tanzania) kwasababu walikosa visa na walikuwa hawajapata ‘passport’”, Tiboroha amefafanua.
“Lakini anamaliza kufanya ‘process’ za passport na nafikiri kesho Niyonzima atafika, hakuna ukweli wa maneno kwamba Niyonzima ameitoroka Yanga”, amesisitiza.
0 comments:
Post a Comment