Friday, July 3, 2015


Mkataba wa Mwashiuya na Kimondo FC

Na Bertha Lumala, Mbeya
MWAKA huu wa Yanga na Kimondo FC! Ni mwaka wao huu! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya leo uongozi wa Kimondo FC kuwaonesha waandishi wa habari nyaraka za mkataba wake na kiungo aliyetua Yanga, Geofrey Mwashiuya.

Wakati mwanzoni mwa wiki ulidai kuwa ulimsajili kiungo huyo akiwa ni mchezaji huru, uongozi wa Kimondo FC umesema una mkataba na mchezaji huyo na utawashtaki mabingwa hao mara 25 wa Tanzania Bara katika mamlaka zinazohusika ikiwa wataendelea kumtumia katika mechi mbalimbali pasipo kumalizana nao.

Mwanzoni mwa wiki Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa mchezaji huyo alisaini mkataba wa miaka mitatu kuitumkia timu hiyo ya Jangwani akiwa ni mchezaji huru.

Hata hivyo, uongozi wa Kimondo FC kupitia kwa mkurugenzi wa klabu hiyo, Elick Ambakisye, umesema kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini hapa leo kuwa Mwashiuya ana mkataba wa miaka minne na klabu hiyo ya Mbeya unaomalizika 2018 aliousaini Agosti 30 mwaka jana.

"Mchezaji (Mwashiuya) mwenyewe alisaini mkataba huu. Endapo Yanga wataendelea kumng'ang'ania na kumtumia mchezaji wetu, tunajua wanashiriki Kombe la Kagame mwezi huu, tutawashtaki katika mamlaka husika," amesema Ambakisye huku akionesha mkataba huo.


Mwashiuya alionesha kiwango kizuri katika mechi yake ya kimataifa ya kirafiki ambayo Yanga ilitoka suluhu dhidi ya SC Villa ya Uganda kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi.

Aidha, uongozi wa Kimondo FC leo umemsainisha mkataba wa miaka miwili aliyekuwa kipa wa Coca-Cola Kwanza ya Kyela, Issa Dickson.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video