Baada ya kuanza vibaya Kombe la Kagame wakifungwa magoli 2-1 na Gor Mahia ya Kenya, mabingwa wa Kandanda Tanzania bara, Young Africans wana matumaini ya kuibuka na ushindi katika mechi ya pili dhidi ya Telcom ya Djibout itakayopigwa kesho majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amefafanua kwamba kocha mkuu wa klabu hiyo, Mholanzi, Hans van der Pluijm na msaidizi wake, Charles Boniface Mkwasa wamejitahidi kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mechi ya ufunguzi iliyopigwa Julai 18 mwaka huu uwanja wa Taifa.
"Kikosi kinaendelea vizuri, walimu wamejitahidi kufanya marekebisho madogo katika kikosi. Tumeona tulivyocheza mchezo wa kwanza, tunakwenda kucheza bila yale mapungufu yaliyojitokeza." Amesema Muro na kuongeza: "Niwahakikishie wapenzi, mashabiki na wanachama wa Yanga popote pale walipo, kesho tunakwenda kucheza vizuri, tunawaheshimu Telecom ambao tunacheza nao, tunaamini tutafanya vizuri".
Wapinzani wa Yanga, Telecom jana walichapwa magoli 5-0 dhidi ya Khartoum ya Sudan.
0 comments:
Post a Comment