BAADA ya kuichapa Khartoum ya Sudan bao 1-0 na kujikuta ikikutana na Azam katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Kagame keshokutwa, Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, ametamba kuwashangaza wapinzani wao hao.
Yanga inakutana na Azam baada ya jana kushinda 1-0 na kushika nafasi ya pili katika Kundi A, huku Gor Mahia walioshika usukani, wakivaana na Malakia ya Sudan kesho jioni, ikiwa ni baada ya APR kukipiga na Khartoum mchana katika hatua hiyo.
Mechi ya kwanza itakayopigwa mchana keshokutwa, itakuwa ni kati ya Al Shandy ya Sudan Kusini na KCCA ya Uganda.
Katika mchezo wa jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga walitawala sehemu kubwa na kukosa mabao lukuki kutokana na washambuliaji wake, hasa Amissi Tambwe aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 30 kutokana na kona ya kiungo Haruna Niyonzima, kukosa nafasi kibao za wazi.
0 comments:
Post a Comment