Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam
Ame Ally, Kipre Tchetche na John Bocco wanataraji kuanza katika safu
ya mashambulizi ya Azam FC wakati itakapo wavaa Yanga SC katika mchezo wa Robo
fainali ya michuano inayoendelea ya Cecafa Kagame Cup 2015.
Timu hizo bora zaidi katika soka Tanzania Bara zitakutana kwa mara ya
pili katika michuano hiyo. Mara ya mwisho zilikutana katika mchezo wa Fainali
miaka mitatu iliyopita na Yanha walishinda kwa mabao 2-0 katika mchezo wa
fainali na kutwaa ubingwa wao wa Tano. MECHI YA LEO..... Azam FC haijaruhusu
goli lolote huku ikiwa imeshinda michezo yote mitatu iliyopita na kufunga mabao
Tisa, wakati wapinzani wao Yanha wanaingia katika mchezo wa leo wakitoka
kushinda michezo mitatu ,mfululizo.
Yanga imepoteza mchezo mmoja kati ya minne iliyokwisha cheza katika
hatua ya makundi. Ikiwa imetoka kundi gumu zaidi katika michuano ya mwaka huu,
mabingwa hao mara mbili mfululizo wa zamani wangependa kuungana na Al Khartoom
na Gor Mahia ambazo tayari zimefuzu kwa nusu fainali.
Timu hizo za Sudan Kaskazini na Kenya zilikuwa kundi A pamoja na
Yanga. BOCCO, AME & KIPRE Walinzi wa Yanga watakutana na washambuaji wa '
daraja la juu Afrika Mashariki na Kati'.
Kipre tayari amefunga mabao Matatu katika gemu tatu zilizopita, wakati
Bocco amefunga mara mbili. Nyota hao wawili wamekuwa wakiifunga Yanga mara kwa
mara na wanaweza kufanya hivyo kwa mara nyingine Jumatano hii na kuipeleka timu
yao nusu fainali. Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub na ' patna wake' Kelvin Yondan
walionekana kupata shida sana wakati walipokutana na GOR ambayo ilikuwa
ikipanga na kufanya mashambulizi ya uhakika siku ya ufunguzi na walionekana '
kuteswa-kimtindo' na kinara wa mabao katika michuano hii, nahodha wa Al
Khartoum, Salh Eldin katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ambao
walishinda 1-0.
Joseph Zuttah na Mwinyi Hajji wamecheza vizuri hadi sasa, walinzi haoo
wa pembeni-Kulia na Kushoto watalazimika kucheza vizuri zaidi wakati
watakapoikabili safu ya mashambulizi ya Azam FC.
Zuttah amekuwa akipandisha timu
kwa mashambulizi ya uhakika akitokea upande wa kulia, Wakati Mwinyi amekuwa
imara, mwepesi na mwenye pasi za uhakika katika beki mbili. Wawili hao ambao
wamechukua nafasi za Juma Abdul na Oscar Joshua wameifanya safu ya ulinzi wa
kati kuwa na utulivu.
Yanga watashambulia kama kawaida yao na watatumia zaidi sehemu za
pembeni ili kufikisha mipira mbele kwa k uwa eneo la katikati ya uwanja
linataraji kuwa ' gumu' kupitisha mipira kutokana na aina ya wachezaji ambao
watacheza sehemu hiyo.
Jean Mugiraneza, Salum Abubakary na Himid Mao wanaweza kuanzishwa kama
viungo watatu wa Azam FC, wakati, Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima na Deus Kaseke
wanaweza kuanza katika nafasi ya kiungo upande wa Yanga.
Azam wamekuwa wakitumia nguvu
zaidi katika idara nyingi lakini wachezaji wao wa nafasi ya kiungo ni wagumu
huku pia wakiwa na ufundi wa kumiliki mpira.
Niyonzima amekuwa akitawala sana mechi dhidi ya Azam FC na safari hii
atakutana na nahodha msaidizi katika timu yake ya Taifa ya Rwanda, Mugiraneza.
Tutaona mpira wa hali ya juu kama wachezaji hawatachezeana rafu za ubabe.
TAMBWE, NGOMA & BUSUNGU, Washambuliaji hao watatu wataanza kwa pamoja
katika safu ya mashambulizi ya Yanga. Tambwe amefunga magoli mawili, Busungu
amefunga mara tatu wakati, Ngoma bado anatafuta goli lake la kwanza klabuni
Yanga. Washambuliaji hao watatu wanaweza kufunga hata magoli mawili na zaidi
katika gemu moja na kufanya hivyo mbele ya safu ya ulinzi ambayo haijaruhusu
goli lolote katika gemu tatu mfululizo itakuwa ni jambo kubwa.
Aishi Manula, Shomari Kapombe,
Erasto Nyoni, Aggrey Morris na Paschal Wawa wamekuwa wagumu kupitika, labda ni
kutokana na aina ya timu walizokutana nazo lakini kiu-alisia, Yanga wanapaswa
kupambana hasa ili kuwa timu ya kwanza kufunga goli dhidi ya Azam katila
michuano hii.
Safu yao ya mashambulizi imefunga magoli lakini bado wanakabiliwa na
tatizo la upotezaji wa nafasi rahisi za kufunga magoli. Wawa amekuwa sababu
kubwa ya ubora wa sasa katika safu ya ulinzi kutokana na uchezaji wake wa
nguvu, uhamasishaji huku akiwa si mchezaji wa kufanya makosa yasiyotarajiwa.
Kapombe tayari amehusika katika magoli mawili ya timu yake. Mlinzi
huyo wa kulia anaweza kuwa tatizo kwa Yanga kutokana na krosi-pasi zake, ni
mchezaji asiyechoka kwenda mbele pale inapohitajika lakini uchezaji wake huo
unaweza kuwa tatizo kwa kuwa, Ngoma si mchezaji wa kumuachia uhuru sana.
Nyoni ameendeleza kiwango chake kizuri na hivyo ataendelea kupangwa
katika kikosi cha kwanza. Atamkabili, Kaseke ambaye amecheza kwa kiwango cha
juu katika gemu nne zilizopita, wakati Wawa na Aggrey watakuwa macho
kuhakikisha, Tambwe na Busungu hawapati nafasi ya kufunga. Nani mshindi wa gemu
hii?. Ni mechi ngumu ila naipa Yanga asilimia 60 za kushinda kutokana na uzoefu
wao wa michuano.
0 comments:
Post a Comment