MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga, wamepewa nafasi kubwa kuweka rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika msimu ujao wa Ligi Kuu, uliopangwa kuanza Agosti 22, mwaka huu kutokana na kufanya usajili ‘bab kubwa’ katika safu ya ushambuliaji.
Ukiachana na washambuliaji hatari waliokuwapo msimu uliopita walioiwezesha Yanga kufunga mabao 52 hadi ligi inafikia ukingoni, klabu hiyo imeongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji kwa kuwanasa Donald Ngoma kutoka FC Platinum ya Zimbabwe, Balimi Busungu, Deus Kaseke na Geoffrey Mwashiuya (Kimondo FC).
Ujio wa Ngoma anayetoka Platinum akiwa na rekodi ya kufunga mabao 29 msimu uliopita, unaweza kuiongezea mabao Yanga na kujikuta ikivuna mabao zaidi ya 75 msimu ujao, kwani hata Busungu aliyefunga mabao 10 msimu uliopita akiwa na Mgambo Shooting, si wa kubeza.
Lakini pia, Kaseke ambaye anapangwa kama kiungo mchezeshaji iwe ni kutokea wingi zote au katikati, anaweza kuwa chachu ya washambuliaji wake kufunga mabao zaidi kutokana na uwezo wake wa kupiga pasi za mwisho, lakini kasi ya kumwezesha kuwasumbua mabeki na hata kufunga pale anapopata nafasi.
Chanzo:Bingwa.
0 comments:
Post a Comment