Yanga jana ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-0 mbele ya Telecom ya Djibouti kwenye mchezo wa kundi A uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa, magoli ya Yanga yakifungwa na Malimi Busungu aliyerudi kambani mara mbili pamoja na Godfrey Mwashiuya aliyefunga goli la tatu.
Mashabiki wa Yanga walikuwa katika nyakati mbili tofauti wakati mchezo wa jana unaendelea, kwanza walianza kwa kushangilia kwa nguvu lakini kadiri muda ulivyozidi kwenda na wachezaji wa Yanga kukosa magoli, mashabiki walianza kupunguza spidi ya ushangiliaji. Lakini baada ya goli la kwanza kufungwa wakalipuka na kushangilia kwa nguvu baada ya hapo walisikika wakizomea hasa Msuva alipokosa penati.
Goli la pili kutoka kwa Busungu na goli la tatu lililofungwa na Mwashiuya yaliwafanya mashabiki kurejea tena kuanza kupiga ngoma na kuimba kuishangilia timu yao kwa nguvu.
0 comments:
Post a Comment