Manchester United wamekuwa wakijaribu kumuuza kisirisiri Robin van Persie, 31, tangu mwezi Januari, kwa mujibu wa mchezaji mwenzake wa zamani Pierre van Hooijdonk (Daily Mirror).
Iwapo ataondoka Old Trafford, klabu ya Besitkas ya Uturuki ingependa kumchukua (Sun).
Manchester United wamekataa pauni milioni 3.5 kutoka Fernabahce za kumnunua Nani (Daily Star), mshambuliaji wa Monaco, Radamel Falcao, 29 amekamilisha utaratibu wa kuhamia Chelsea (Guardian).
Manchester City wanakabiliwa na ushindani mkali zaidi kumsajili kiungo wa Juventus Paul Pogba, huku Barcelona wakitoa pauni milioni 56.7. City wana matumaini ya kumsajili Kevin De Bruyne kutoka Wolfsburg (Daily Mail).
Kipa wa Arsenal Wojciech Szcesny, 25, 'alidanganywa' na Arsene Wenger kuhusu hatma yake Emirates na usajili wa Petr Cech, kwa mujibu wa kipa wa zamani wa Poland Jan Tomaszewski (Przeglad).
Aston Villa wanajiandaa kutoa pauni milioni 6.5 kumsajili Msenegali Idrissa Gueye, hatua ambayo itasababisha kuondoka kwa Fabian Delph, 25 (Sun).
Mshambuliaji Thomas Muller, 25, amesema "yuko poa Bayern Munich" baada ya taarifa kuibuka kuwa Manchester United wametoa mkataba wenye thamani ya pauni milioni 120 (Daily Express). Chelsea watapanda dau hadi pauni milioni 8 kumchukua kipa wa Stoke City Asmir Begovic, 28 (Daily Telegraph).
Liverpool wanakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Aston Villa Christian Benteke 24 (TalkSport).
Dau la pauni milioni 20 la Manchester United kumtaka Morgan Schneiderlin limekataliwa na Southampton (Daily Telegraph).
Chelsea wanataka Atletico Madrid walipe pauni milioni 14.25 kumchukua Filipe Luis (The Sun), Manchester United watampa Sergio Ramos mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya pauni milioni 39 baada ya kukata kodi, kitita ambacho Real hawawezi kutoa (Cadena SER).
Manchester City wapo tayari kutoa pauni milioni 25 kumchukua winga wa Bayer Leverkusen Karim Bellarabi (The Sun).
Bastian Schweinsteiger hatojiunga na Manchester United na atasalia Bayern hadi mkataba wake utakapomalizika 2016 (Bild).
Stoke wanajiandaa kumpa mkataba Xherdan Shaqiri, 23 baada ya kukubaliana ada ya uhamisho ya pauni milioni 12 na Inter Milan (Times).
0 comments:
Post a Comment