Sunday, July 26, 2015

Na Nicasius Nicholaus Agwanda (Nicasius Coutinho Suso) 

Wakati ligi nyingi zikiwa katika mapumziko za michezo mbalimbali, pacha wa ligi kuu ya kikapu nchini Marekani (NBA) hapa tunaongelea ligi kuu ya kikapu ya wanawake Marekani maarufu kama WNBA imekuwa ikiendelea kama kawaida. Na kama ilivyo kwa Kaka zao huwa kunakuwa na tukio linaloitwa ALL STAR BREAK, ambapo nyota mbalimbali wa vilabu tofauti upigiwa kura na kutengeneza timu mbili za Kanda tofauti yaani Magharibi na Mashariki na kufanya mchezo mmoja wa Ushindani baina yao, na Hii imekuwa ni moja ya tamaduni maarufu kwa michezo mingi nchini Marekani.
Wakati katika All star ya wanaume mshindi akiwa ni Kanda ya Magharibi kwa mwaka 2015, na mchezaji bora siku hiyo ama mchezaji alopewa tuzo ya thamani kwa mchezo huu akiwa ni Russell Westbrook wa Oklahoma City Thunder katika WNBA All Star iliyofanyika Jana siku ya Jumamosi 25 July, timu ya wanawake ya Kanda ya Magharibi iliweza kuwashinda wenzao wa Mashariki kwa jumla ya vikapu 117 dhidi ya 112. Mchezaji wa Minnesota Lynx ambaye pia ndiye aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora ama mwenye thamani kwa msimu uliopita wa WNBA, Maya Moore alifanikiwa kushinda tuzo ya Mchezaji bora wa All Star mwaka huu baada ya kufunga vikapu 30 peke yake.  Hata hivyo Kuna baadhi ya rekodi ziliandikwa.
1. Tamika Catchings ameweka rekodi ya kuwa mfungaji wa Muda wote wa WNBA all star akimpita Lisa Leslie aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo na Sasa Ana point 108. Ikumbukwe Tamika Catchings alisema msimu ujao ndo utakuwa msimu wake wa mwisho WNBA na kwakuwa katika misimu inayohusisha Olympics huwa hakuna WNBA all star ni wazi Tamika hatocheza tena All star nyingine. Mwenyewe amenukuliwa akisema Ligi inabaki katika mikono salama kwani Kuna wachezaji wengi wadogo wenye vipaji akitolea mfano wa Maya Moore,  Britney Grinner na Ellena Della Done.
2. Kulikuwa na wachezaji 10 waliocheza kwa mara ya kwanza all star, idadi kubwa zaidi tangu mwaka 2011.
3. Mchezaji Elena Delle Donne ndiye aliyeingia kwa Kupigiwa kura,  naye ilikuwa mara yake ya kwanza lakini alikosa michuano miwili iliyopita kwa majeruhi. Jambo jingine la kuvutia ni kuwa alivaa viatu maalumu vilivyobuniwa na mwanafunzi wa chuo Matthew Walzer, ambaye aliwataka Nike kutengeneza viatu maalumu kwa ajili ya Walemavu na wasiojiweza na Delle Donne alimuunga mkono kutokana na kuwa na dada yake mwenye ulemavu wa akili, upofu na kiziwi.
4. Mwanadada  Plenette Pierson, alicheza mchezo wake wa kwanza wa WNBA all star lakini ikiwa ni katika msimu wake wa 13 katika ligi hiyo.
5. Maya Moore alivunja rekodi ya vikapu au point nyingi zaidi kufungwa na mchezaji mmoja katika. Mchezo mmoja WNBA All Star. Point 30 alizofunga zilizipita zile 29 za Shoni Schimmels.
6. Tamika Catchings pia ameweka rekodi ya kucheza michezo msingi zaidi ya WNBA All Star (10) akivunja rekodi ya mwanadada Tina Thompson.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video