Ni wakati ambao msimu mpya wa EPL unakaribia kuanza, hivyo timu nyingi zipo katika harakati za kuzindua jezi zao mpya kwa ajili ya msimu utakaoanz ahivi karibuni.
Wakati baadhi ya vilabu vikitumia muda mwingi katika kutambulisha jezi zao mpya kwa mwaka 2015/16 kwa njia ya video, lakini, West Brom kwa upande wao wamekuja kivingine kabisa.
Wametoa video ambayo kwanza ni fupi, si zaidi ya dakika moja ambayo muda mrefu imeonesha tukio la mchezaji Gareth McAuley alipotolewa nje kimakosa katika mchezo dhidi ya Manchester City msimu uliopita, na baadaye ndipo walipoonesha kipande cha video chenye utambulisho wa jezi mpya za nyumbani na kuongeza na maelezo yaliyosika; "Jezi hizi mpya nadhani zitakuwa rahisi kutambulika.”
0 comments:
Post a Comment