Saturday, July 25, 2015

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa Mkurugenzi wa klabu hiyo Lord Harris ameongeza chumvi kuhusu uwezo wa kifedha wa klabu katika suala la usajili msimu huu.
Lord Harris alisema kuwa Arsenal ina uwezo mkubwa wa kifedha kwa sasa kununua mchezaji wa aina yoyote isipokuwa Lionel Messi na Christiano Ronaldo, kutokana na kuwa na kiasi cha zaidi ya pauni milioni 200 katika akaunti.
"Lord Harris kwa kiasi fulani ameenda mbali sana kwa sababu hakuna ukweli wowote juu ya hilo",aliwaambia waandishi.
"Tupo kaika nafasi ambapo tuko makini kuangalia kama kuna mtu sahihi atapatikana, basi tunaweza kufanya kitu, lakini si kama ambavyo imezungumzwa.
"Tuko katika nafasi nzuri kabisa tukiwa na kikosi bora, mimi nina furaha kwa hilo.
"Sisi tuko makini kwa kila sehemu. Tuko makini kutafuta wachezaji tunaoweza kuwapata. Tumetumia kiasi kikubwa sana fedha mismu miwili iliyopita na kumleta Gabriel katikati ya msimu ambaye yuko tayari kwa mapambano sasa.
"Hatukatai kutumia pesa katika kusajili. Kwa sasa pesa ipo, endapo tutampata mchezaji sahihi basi tutatumia hela".

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video