Arsene Wenger ameweka wazi mpango wake wa kumpa Mesut Ozil fursa ya kudumu kucheza namba kumi kuanzia msimu ujao wa ligi kuu nchini Uingereza na mashindano mengine.
Ozil, ambaye tangu asajiliwe kutoka Madrid hajaonesha kiwango kilichotarajiwa na wengi, atapewa nafasi hiyo ili kurudisha makali yake kama alivyokuwa akifanya Madrid.
Nyota huyo wa Ujerumani amekuwa mara kadhaa akichezeshwa nafasi tatu tofauti na Wenger hali ambayo hata yeye mwenyewe alionekana kutofurahishwa nayo.
0 comments:
Post a Comment