Waziriwa wa Utamaduni, Vijana na Michezo wa Sudani Kusini Mh. Stephen Lado Onesimo jana aliitembelea timu ya Malakia FC wakati ikifanya mazoezi kwenye uwanja wa Karume wakati ikijiandaa kwa ajili ya mchezo wake wa leo dhidi ya KCCA ya Uganda mchezo utakaopigwa majira ya saa 8:00 mchana kwenye uwanja wa Taifa ikiwa ni mwendelezo wa mashindano ya Kagame Cup hatua ya makundi.
Waziri huyo amesema, wachezi wa Malakia wanahitaji kushinda mchezo huo japo tayari wananafasi ya kucheza hatua ya robo fainali lakini ushindi kwenye mchezo huo utazidi kuwajengea heshima kwenye soka la ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati lakini pia watakuwa wanaweka heshima ya nchi yao (Sudan Kusini) ambayo imekuwa ikibezwa kwenye soka tangu ijitenge kutoka Sudan (Kaskazini).
Mchezo wenu dhidi ya KCCA ni muhimu sana ndiyo maana nimekuja hapa kuzungumza na ninyi ili kuhakikisha mnashinda mchezo huo na kujiwekea heshima nyinyi wachezaji na klabu yenu lakini kubwa zaidi ni nchi yetu ya Sudan ambayo imekuwa ikibezwa kwenye michezo hasa soka tangu tujitenge kutoka Sudan”, alizungumza kwa hisia.
“Nitakuwepo pia uwanjani kuwashuhudia mkicheza mchezo wenu, nahitaji mjitume kwa ajili ya nchi yetu ya Sudan na endapo mtashinda mchezo wenu, nawaahidi kuwapa zawadi. Nimezungumza na kocha wenu ameniambia tayari mnanafasi ya kucheza robo fainali ya mashindano haya, lakini mimi nahitaji mshinde mchezo huu ili mkacheze robo fainali mkiwa mnaheshimiwa”, alisisitiza.
“Nidhamu kwenye mchezo ni kitu muhimu sana, kila mtu anatakiwa awe na nidhamu ya hali ya juu wakati wa mchezo, muelekezane wenyewe kwa wenyewe muwapo uwanjani nani anatakiwa kufanya nini ili kumpunguzia kazi kocha wenu. Mimi nawatakia kila kheri na ninaimani na ninyi na ninamatumaini tutashinda mbele ya KCCA”, alimaliza.
Malakia ilishinda mchezo wake wa kwanza mbele ya Adama City lakini ikapoteza mchez wake wa pili dhidi ya Azam FC, leo inaingia uwanjani kuikabili KCCA hata kama itapoteza mchezo wa leo itaingia kucheza robo fainali ya Kagame kama best loser. Mchezo mwingine wa kundi hilo (Kundi C) utakuwa ni kati ya Azam FC dhidi ya Adama City utakaochezwa kuanzia saa 10:00 jioni kwenye uwanja wa Taifa.
0 comments:
Post a Comment