Kikosi cha Gor Mahia
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
MABINGWA wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) Gor Mahia wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika hatua ya mtoano ya michuano ya Kombe la Kagame itakayofanyika jijini hapa kuanzia Julai 18.
Mabingwa hao mara tatu wa michuano hiyo ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) walitwaa taji la mwisho 1985 na wamepanga kufanya kweli awamu hii baada ya kutolewa hatua ya makundi mwaka jana mashindano hayo yalipofanyika Rwanda.
Gor Mahia imepangwa Kundi A pamoja na wenyeji Yanga, El Khartoum ya Sudan, Telecom ya Djibouti na KMKM ya Zanzibar. Timu itakayoshinda mechi kuanzia mbili itakuwa na uhakika wa kusonga mbele kuingia hatua ya robo fainali ambapo kundi hilo litatoa timu tatu.
Timu mbili kutoka Kundi B na C zitasonga mbele wakati timu moja miongoni mwa timu nne zinazobaki itapata nafasi ya 'best loser' kutoka Kundi B na C.
Macho yote yataelekezwa kwa Gor Mahia ambayo imemaliza mzunguko wa kwanza wa KPL msimu huu bila kupoteza mechi hata moja.
Kundi A - Gor Mahia (Kenya), Yanga (Tanzania), KMKM (Zanzibar), Telecom (Djibouti), El Khartoum-(Sudan).
Kundi B – APR (Rwanda), Al Shandy (Sudan), LLB FC (Burundi), Heegan (Somalia).
Kundi C – Azam (Tanzania), Malakia (South Sudan), Adama City (Ethiopia), KCCA(Uganda).
0 comments:
Post a Comment