Done Deal: Chelsea imethibitisha kumsajili kipa huyo, huku ikisema kuwa imefurahi kumpata mlinda mlango huyo anayekuja kuziba nafasi ya Petr Cech aliyetua Arsenal majira haya ya kiangazi na huo ni usajili wa pili baada ya kumnasa Radamel Falcao.
Nayo Stoke City imetangaza kwamba golikipa wake Asmir Begovic amesajiliwa na Chelsea kwa mkataba wa miaka minne.
Begovic mwenye miaka 28 amejiunga na Chelsea kwa ada inayoaminika kuwa paundi milioni 8.
Hata hivyo Begovic anaweza kujikuta akikaa benchi kwa msimu wa 2015-16 kwasababu Thibaut Courtois amejiimarisha kama kipa chaguo la kwanza Stamford Bridge.
0 comments:
Post a Comment