Thursday, July 23, 2015

Manchester United wamekubali ofa ya Euro milioni 65 kumuuza Angel Di Maria katika klabu ya Paris Saint-Germain (PSG), hii ni kwa mujibu wa France Football.
Imeripotiwa kwamba siku chache zilizopita Mkurugenzi mkuu wa Man United,  Ed Woodward  alikuwa na mazungumzo na Mkurugenzi msaidizi wa michezo wa PSG, Olivier Letang ambapo wamefikia makubaliano ya ada ya uhamisho ya winga huyo wa zamani wa Real Madrid ambaye anaondoka Old Trafford baada ya kudumu kwa mwaka mmoja tu katika soka la England.
Inafahamika kwamba PSG wanataka kukamilisha dili hilo kabla ya wikiendi ili Muargentina huyo aliyesajiliwa mwaka jana na Man united kwa paundi milioni 59.7 ajiunge na wachezaji wenzake waliopo katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya nchini Marekani.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video