Sunday, July 12, 2015

Mambo vipi wapenzi wa spoti hasa wale wa soka, ukiachilia mbali maswala ya siasa ambayo yanatikisa kwa sasa hapa "Bongo" hebu fanya  kuyapotezea kidogo na kwa muda huu tuangalie habari fulani za kufurahisha ama kushangaza kidogo katika soka,

Kwa mara ya kwanza Sweden ilimfahamu "Ibra-Kadabra"  katika Timu ya soka ya  FBK Balkan ambayo Zlatan Ibrahmovic alianza kuichezea tangu akiwa mdogo, ikiwa nyuma kwa magoli 4-0, Zlatan  alipokuja kipindi cha pili aliweza kufunga magoli 8 na kuiwezesha timu yake kushinda 8-4.


kumbuka Zlatan alikuwa hachezeshwi kipindi cha Kwanza kutokana na ukorofi wake na Kocha Mkuu wa Balkan alikuwa mwoga sana kumpanga Zlatan kwani mara nyingi alikuwa akipewa kadi na kuigharimu
timu yake ya vijana. Upo hapo? Ulizani Zlatan kaanza ukorofi ukubwani?

Nitakuwa sijakutendea haki kama sitakukumbusha hili, Ebwana ni kwamba aliyekuwa mchezaji wa Manchester United, Ryan Gigs ndio mchezaji wa kwanza katika "premier league" kufunga magoli 100 bila hatrick hata moja, Najua unapata shaka kuamini hili ila huo ndo ukweli, kumbuka Baba yake Gigs ana asili ya Sierra Leone japokuwa ni raia wa Wales.

Pia mchezaji bora wa dunia mara mbili 2004 na 2005, Ronaldinho Gaucho Kwa mara ya Kwanza aliviteka vyombo vya Habari vya dunia pale timu yake ya vijana iliposhinda 23-0 huku akifunga magoli yote. Ndio,  huyo ndo Gaucho, bila shaka wengi mnamkumbuka kwa chenga za mauzi na "dribbling" zake za kufurahisha. Kumbuka baada ya tukio hili klabu ya soka ya Gremio ilimuona na  kumchukua.

Wakati mwingine katika soka kuna habari ambazo ukizisikia lazima utashangaa na kama wewe ni mvivu wa kusoma lazima utabisha tu, sasa chukua hii, umri Kati ya Lionel mess na mwenzake Christiano Ronaldo ni siku 869, Lakini tofauti hiyo hiyo ndio kati ya watoto wao wa kiume, Thiago na Ronaldo Junior.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video