Tuesday, July 14, 2015

ZOEZI la usajili kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara linaendelea kwa sasa nchini na limewanufaisha baadhi ya wachezaji ambao kwa namna moja au nyingine, wala hawakuota kuangukiwa na zali. Unajua ni zali gani? Wapo baadhi ya wachezaji hawakuota kama wangekuja kucheza michuano ya Kombe la Kagame, lakini ni usajili unaoendelea ndio umewapa zali hilo. Wachezaji hao kama wangebaki katika klabu zao ingekuwa vigumu kwao kuicheza michuano hiyo inayoshirikisha Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati itakayoanza mwishoni mwa wiki hii jijini Dar es Salaam. Hii ni kwa sababu klabu zao hazina sifa za kushiriki michuano hiyo.
Mwanaspoti linakuorodheshea wachezaji wachache walioangukiwa na bahati ya kuicheza michuano hiyo ya mwaka huu bila kutarajia.
Ramadhani Singano-Azam
Ametua Azam FC wakati ikijiandaa na michuano ya Kagame, hivyo ni wakati mzuri kwake kujaribu bahati yake ya kuonyesha kiwango kwa timu za nje.
Wakati mwingine mgogoro wake na timu yake ya zamani Simba, umemsaidia yeye kumpa hatua nyingine, ni wazi kama angekuwa katika klabu yake ya zamani basi angekuwa mtazamaji kwani Simba haishiriki michuano hiyo kwa miaka mitatu sasa.
Malimi Busungu-Yanga
Ni lazima amshukuru Mungu kwa kusajiliwa kwake Yanga ambayo imepata nafasi ya kushirikiki Kagame kwani angekuwa Mgambo JKT, timu yake ya zamani basi angekuwa anaisikia michuano hiyo hewani ama wakati mwingine angekuwa anatazama wenzake wakifanya kazi.
Akiitumia vyema nafasi atakayopata Yanga, basi ni dhahiri ndoto yake inaweza kupenya umbali mrefu hasa kwa timu zinazoshiriki michuano hiyo.
Geofrey Mwashiuya
Kweli mwenye bahati habahatishi kwani ni adimu sana mchezaji kung’ara kutoka timu ya Ligi Daraja la Kwanza kisha akatikisa kwenye klabu kongwe kama Yanga, haikuwa rahisi kwake kuwa mmoja wa wachezaji wanaotarajiwa kucheza Kagame.
Mchezaji huyo kutoka Kimondo ya Mbozi, ametua Jangwani na mguu wa bahati kwani ameingia Yanga wakati ikijiandaa na michuano hiyo na ni muda mwafaka kwake kuonyesha uwezo wake katika michuano hiyo ya Kagame.
Deus Kaseke-Yanga
Amebahatika kusajiliwa Yanga ambayo inashiriki michuano ya Kagame inayotarajiwa kuanza Jumamosi na kikosi chake kitafungua pazia la michuano hiyo dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.
Kiwango chake ndicho kilichomchomoa Mbeya City ambayo haipo kwenye michuano hiyo ingawa wadau wengi walitarajia huenda ingeshiriki kutokana na Tanzania Bara kuwa wenyeji hivyo walitarajia wangetoa timu tatu nayo ingekuwepo. Kama angeamua kuongeza mkataba Mbeya City ni wazi ingekula kwake na asingepata bahati ya kushiriki michuano hiyo. Hivyo ni nini kama si zali la mentali kama alivyowahi kuimba Profesa Jay na Sir Juma Nature?
Ame Ali-Azam
Wenyewe wanamwita Zungu. Alikuwa Mtibwa Sugar ambayo ilianza Ligi Kuu msimu uliopita kwa mkwara kabla ya kutepeta.
Kama angesalia katika timu hiyo ya Wakata Miwa, ni wazi asingepata nafasi ya kuuza sura Kagame, lakini kusajiliwa kwake na Azam kunampa uhakika wa kulitangaza jina lake kama atafanya mambo makubwa.
Kutua kwake Azam, kunampa Zungu nafasi ya kufanya yake akishirikiana na wachezaji wenzake chini ya kocha Stewart Hall.
Zungu ni bonge la mchezaji na kama asingepata nafasi hiyo ndani ya Azam, angekuwa mtazamaji wa kuwaangalia wenzake wakifanya yao kwa raha zao.
Haya tusubiri tuwaone uwanjani.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video