Tuesday, July 7, 2015


Baada ya kimya kirefu kutanda kuhusu hatma ya winga wa Yanga Simon Msuva na hatma ya majaribio aliyofanya kwenye klabu ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini, meneja wake Mohamed Msemo ameibuka na kufunguka kuhusina na ukimya huo unaozua utata kwa mashabiki wengi wa soka.
Mohamed Msemo amesema wakala liyeondoka na Msuva kumpeleka kufanya majaribio kwenye klabu ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini hajasema lolote tangu winga huyo wa Yanga arejee nchini baada ya kufanya majaribio na yeye (meneja) haoni sababu ya kuendelea kufatilia jambo hilo kwasababu wao ndio walikuja kumtaka mteja wake na endapo wanaona anawafaa, basi watakuja kufanya mazungumzo.
“Yule mtu aliyekuja kubisha hodi kwetu akasema anamuhitaji Simon Msuva aliondoka nae akaenda nae Afrika Kusini kufanya nae majaribio kule. Alipomaliza tulimwambia aje atupe majibu ya mtoto (Msuva) baada ya kufanya mazoezi nini matokeo yake, auambie uongozi wa Yanga kama Msuva alifuzu majaribio na kama wanamuhitaji au la”alisema Msemo.
“Lakini mpaka sasahivi wako kimya na mimi nimemwambia Msuva aendelee na mwajiri wake (Yanga) mpaka watakapo sema lolote kwasababu sisi Tanzania tusijifanye kwamba tupo chini sana, kama wanamuona anathamani kwao watakuja watatuambia lakini sio sisi twende kuwaulizia”, ameongeza.
“Wao ndio walimtaka, wakasema tumempenda huyu kijana na wakaenda kufanya nae majaribio, walitakiwa waje sasa wauambie uongozi wa Yanga kwamba,  tumemuona kijana wenu, tumempenda na tunamuhitaji tufanye biashara. Kama wao hawajasema hivyo sisi hatuwezi kwenda kusema mlishamuona sasa mnasemaje”, alifafanua.
Mwishoni mwa msimu wa ligi iliyopita Msuva aliondoka kwenda Afrika Kusini kufanya majaribio kwenye klabu ya Bidvest Wits lakini tangu amerudi nchini hakujawa na taarifa yoyote inayosema kwamba Msuva alifanikiwa kufuzu majaribio hayo na mipango gani inaendelea au kama alishindwa kufuzu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video