Na Ramadhani Ngoda.
Wakala wa Mlinda mlango wa klabu ya Real Madrid na
timu ya tifa ya Hispania, Iker Casillas, Carlo Cutropia ameweka wazi kuwa
mteja wake anataka kutimkia kunako klabu ya Porto inayoshiriki ligi kuu nchini
Ureno anakoona atapata nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza.
“Casillas anavutiwa na ana shauku na kujiunga na Porto,”
alisema wakala huyo kukiambia chombo kimoja cha habari.
Nafasi ya mlinda lango huyo imekuwa mashakani baada ya Madrid
kuwa mbioni kunasa saini ya mlinda lango wa Manchester United, David De gea anayeonekana
kuwa wake mbadala sahihi Santiago Bernabeu.
Casillas (34) aliyeichezea Madrid Zaidi ya michezo 700 (katika
mashindano yote) tangu alipoingia rasmi kwenye kikosi cha kwanza msimu wa
1999/2000, ana Imani kuwa klabu hiyo itamfungulia mlango wa kutokea na kumpa Baraka
zote aendapo.
“Tuna Imani Madrid watamruhu kuondoka bila shaka yoyote,”
aliongeza wakala huyo.
Casillas anafikia uamuzi wa kuondoka Madrid licha ya kuwa na
kandarasi na miamba hiyo ya Hispania mpaka Juni 2017.
Mpaka sasa amekwisha shinda mataji 5 ya La Liga, mataji 2 ya
Copa Del Rey, pamoja na kushinda Super copa De Espana mara 4 bila kusahau ligi
ya mabingwa Ulaya alioshinda mara 3, Super Cup mara 2 na kombe la dunia kwa
vilabu (FIFA Club world cup).
0 comments:
Post a Comment