Sergio Aguero na wenzake wengine raia wa Amerika Kusini wanaokipiga Manchester City watakosa mechi za mwanzo za msimu wa EPL, amesema Manuel Pellegrini.
Aguero, Pablo Zabaleta, Martin Demichelis na Fernandinho bado hawajaungana na wenzao katika mechi za maandalizi ya msimu mpya kutokana na kuongezewa muda wa kupumzika baada ya kumalizika kwa michuano ya Copa America huko nchini Chile.
"Nadhani katika mchezo wa soka ni muhimu sana kufanya kucheza kwa bidii, hivyo basi waliobaki pia wana umuhimu sawa na wengine", Pellegrini aliwaambia waandishi.
"Una mechi nyingi sana katika msimu mzima, ambapo endapo kama hutowapa siku 30 za mapumziko baada ya kumalizika kutumikia mataifa yao, ni vigumu sana kwao kuweza kuwa na nguvu ile ile katika msmu mzima.
"Ni zaidi ya vigumu hasa kwa wachzaji wa Amerika Kusini kwa sababu Pablo Zabaleta, Martin Demichelis, Sergio Aguero na Fernandinho wametoka katika timu zao za taifa hivi karibuni, hivyo hawatakuwa na siku 30 za mapumziko.
"Nadhani watakaporudi klabuni hapa wataanza maandalizi kwa ajili ya msimu mpya, pengine hawatojumuishwa katika michezo ya mwanzo, lakini nina imani kubwa kuwa watafanya kazi kwa juhudi ili kujiweka sawa mapema iwezekanavyo."
0 comments:
Post a Comment