Friday, July 24, 2015


Nilipata taarifa kuwa Samata kakataa dau la Waarabu.... nilimuona mjanja sana maana pale angekuwa ni sawa amebadili chupa ila mvinyo ni ule ule..!!! vipi na hapa kwenye ardhi ya madafu usajili gani umetikisa? wa Okwi au..! Mwashiuya je...! lakini mbali na usajili wa
Azam, Simba na Yanga, kuna sajili zingine nyingi na nzuri ambazo hazizungumzwi kabisa, anyway tuachane na hayo japokuwa leo sijakugusia siasa japo kwa mbali..! ila fahamu ya kwamba Obama yupo Kenya na ametoka "White house" ambapo "amemzingua" yule M-nigeria kumpa silaha kuwaumiza "Boko haram", ndo ujue ugaidi kwanini hauishi duniani...

Liverpool imesajili mshambuliaji mzuri na mkubwa ambaye alikuwa anacheza timu ndogo na ya kawaida, sina haja ya kuzungumzia kiufundi maana wachambuzi wameshazungumzia sana, ila leo naomba umfahamu japo kwa uchache Christian Benteke, mshambuliaji ambaye amefunga magoli 49 katika mechi 100 ila hazungumzwi sana, lakini angekuwa Raheem au Walcott kafanya hivyo ungesikia "Sky sport" au "ESPN" wanamuandika kwenye vyombo vyao "World Class Striker" ila tuyaache hayo leo nimekuwekea vitu vichache ambavyo pengine huvijui
kutoka kwa Christian..

Usajili wa Christian Benteke kutoka Villa park kwenda Anfield ndio biashara ghali ya usajili kuwahi kufanywa na Aston villa tangu timu hiyo ianzishwe mwaka 1874.

Christian Benteke mwenye umri wa miaka 24, alizaliwa Zaire {D R C} katika jiji la Kinshasa, alihamia Belgium yeye na familia yake kwa lengo la kuukwe utawala wa Mobutu.

Tofauti kabisa na wachezaji wengine, Christian Benteke anaamini Thierry Henry ndo mchezaji wake bora mpaka sasa na anatamani siku moja akanyage Mafanikio aliyoyapita Thierry Henry.

Katika usajili uliofanywa na Aston villa majira ya kiangazi mwaka 2012, Benteke alikuwa mchezaji wa nane kusajiliwa pale Villa park nyuma ya Karim El Ahmadi (£2m), Brett Holman (free), Matthew Lowton (£3m), Ron Vlaar (£3.2m), Joe Bennett (£2.75m), Jordan Bowery (£500,000) na Ashley
Westwood (£2m).

Anapenda sana Basketball na mara kibao katika "interview" zake amesikika akisema yeye ni shabiki wa kutupwa wa Cleveland Cavaliers na ametokea kuipenda timu hiyo Kwasababu ya LeBron James.

Mnamo tar 15 September 2012, Benteke alifunga goli lake la Kwanza pale EPL dhidi ya Swansea city akitokea "sub" baada ya hapo alikaa dakika 343 bila kufunga, ila baadae alikuja kuwa "mtamu" zaidi ya "mcharo" katika ufungaji.

Benteke kama ni mshambuliaji, lakini pia anae mdogo wake anaecheza kwenye klabu ya Zulte Waregem inayoshiriki ligi ya Belgium ambaye nae anacheza nafasi ya ushambuliaji.

Baada ya kutua Villa park kwa kitita cha £7m, alitamka maneno machache sana, "hatimaye nimetimiza ndoto zangu"

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video