Friday, July 31, 2015


Michuano ya CECAFA inazidi kushika kasi katika ardhi ya jiji la Dar es salaam, bila shaka timu ambazo zimefika kwenye hatua hii zinastahili kupewa heshima kwani haikuwa kazi nyepesi kuvuka huko nyuma waliokotoka.
 Mabingwa wa Kenya ni miongoni mwa timu ambayo
inazungumziwa sana na wanasoka mbalimbali hasa kutokana na soka wanaloonesha pamoja na kumailza vizuri kwenye makundi huku pia wakifanya vyema kwenye hatua ya robo fainali.
Leo wameshinda magoli 3-1 dhidi ya Al Khartoum na kutinga fainali ya kombe la Kagame.
Sio mbaya tukitazama baadhi ya vitu ambavyo pengine hukuwahi kudhani ama kufikiri juu ya klabu hii inayopatikana nchini Kenya.

Gor mahia kwa mara ya kwanza ilianzishwa mwaka 1910 ila ilisajiliwa na kuwa klabu rasm mnamo February 17 1968 baada ya kuungana kwa Luo union na Luo sport club {iliyokuwa Luo stars}

Miongoni mwa viongozi wa klabu hii kubwa kwenye ukanda wa CECAFA ni hayati Tom Mboya {mzalendo na kiongozi wa kenya, ni miongoni mwa watu waliopigania uhuru wa Kenya} na Jaramogi Oginga Odinga, aliyekuwa chifu wa Kijaluo na baadae kuwa makamu wa kwanza wa rais, kumbuka huyu
ndio baba yake kiongozi wa upinzani nchini kenya kwa sasa Raila Odinga.

Mwaka 1976, Gor mahia ilichukua ubingwa wa ligi bila kupoteza mechi yoyote, hapa wanaungana na timu kibao barani Africa zikiwemo Simba na Asec Memosa. Mpaka sasa pia hawajapoteza mechi kwenye ligi.

Katika ukanda wetu wa mashariki mwa Africa, Gor mahia ndio timu pekee iliyo wahi kushinda ubingwa wa kombe la shirikisho {zamani kombe la washindi} hii ilikuwa mwaka 1987 kabla ya hapo mwaka 1979 ilifika fainali, lakini imezizidi simba na yanga kwani hata kwenye hatua ya
robo fainali imefika mara kadhaa. Simba na Yanga waliwahi kujaribu kuchukua ubingwa ila juhudi zao ziligonga mwamba.

Mwaka 1996 Gor mahia ilitolewa kwenye raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa barani Africa na klabu ya Dynamo ya zimbwabwe, hali hi ilipelekea fujo mbaya sana uwanjani na kutokana na matokeo hayo mechi za soka hazikufnyika pale Nairobi kwa muda Fulani.

Kwa mara ya kwanza mwaka 2001, Raj Binder Singh alikuwa mtu wa kwanza mwenye asili ya ki asia kuiongoza klabu ya gor mahia, kumbuka huyu jamaa alikuwa mwenyekiti wa klabu hii yenye wafuasi wengi sana pale kenya.
 Kwa hapa “bongo” viongozi wenye asili ya ki asia kuongoza
vilabu vyetu ni hali ya kawaida na imeanza muda mrefu kidogo. Mwaka 2002 Gor mahia ilimailiza ligi ikiwa na tofauti ya magoli {-20}, pia mwaka 2006 ilikataa na kudharau faini waliyopigwa na KPL, hali hii iliwaletea matatizo sana lakini baade mambo yalikwenda sawa.

Pia kumbuka wapinzani wao wa jadi pale nchini kenya ni Afc Leopard, Gor mahia imeshinda ubingwa wa ligi ya kenya mara nyingi kuliko timu yoyote pale kenya, imechukua ubingwa mara 14 mpaka sasa.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video