Friday, July 24, 2015

DEUS Kaseke, Malimi Busungu na Geoffrey Mwashiuya wameunda utatu hatari ndani ya kikosi cha Yanga ambao huenda ukawa moto wa kuotea mbali kwa timu pinzani, lakini iwapo hawatalewa sifa wanazozipata kutoka kwa mashabiki.
Wachezaji hao ambao leo wanatarajiwa kuendeleza makali yao watakapoivaa KMKM ya Zanzibar katika mchezo wao wa Kombe la Kagame, Uwanja waTaifa, Dares Salaam, juzi waliibuka mashujaa wa Yanga kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Telecom ya Djibouti.
Watatu hao ambao wote wamesajiliwa mwishoni mwa msimu uliopita, tayari wameonekana kukonga nyoyo za watu wa Yanga kutokana na uwezo wanaouonyesha uwanjani.
Katika mchezo wa juzi, Kaseke alionyesha kiwango cha hali ya juu akikaba bila kuchoka, kupora mipira na kusaidia mashambulizi kitendo kilichoonekana kuwakuna mno mashabiki wa timu yake.
Kwa upande wake, Busungu aliyefunga mabao mawili, naye alifanikiwa kuwateka watu wa Yanga kutokana na kung’ara na kuwafunika washambuliaji wa kigeni, Kpah Sherman na Amiss Tambwe ambao walitoka kapa.
Mwashiuya aliyeingia mwanzoni mwa kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Tambwe aliyetolewa baada ya kukosa penalti, alifanya kile kilichowasukuma mashabiki kupiga kelele kutaka aingizwe pale alipotoa mchango mkubwa kupatikana kwa bao la pili na la tatu.
Chanzo:Bingwa

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video