Raheem Sterling leo amefunga goli lake la kwanza ndani ya dakika tatu akiichezea Manchester City dhidi ya AS Roma.
Man City wameshinda kwa penalti 5-4 baada ya kutoka sare ya magoli 2-2.
Ulikuwa mtihani mkubwa kwa Sterling kuwathibitishia Manchester City kwanini wamelipa paunndi milioni 49 kumsajili kutoka Liverpool majira haya ya kiangazi na kwa dakika chache alizocheza amejitahidi kuonesha ufundi.
Moja ya stori kubwa ni Sterling kuanguka mwenyewe baada ya kukanyaga juu ya mpira akijaribu kukokota ii amtoke beki wa Roma, Alessandro Florenzi.
Mashabiki wa Roma waliokuwa wanamzomea wameonekana kushangulia tukio hilo
Tazama Jinsi Sterling alivyoanza kukipiga Man City
MIKWEAJU YA PENALTI
Yaya Toure (Man City) - alifunga
Radja Nainggolan (Roma) - alifunga
Aleksandar Kolarov (Man City) - alikosa
Adem Ljajic (Roma) - alifunga
Jesus Navas (Man City) - alifunga
Mattia Destro (Roma) - alifunga
Marcos Lopes (Man City) - alifunga
Iago Falque (Roma) - alifunga
Joe Hart (Man City) - alifunga
Seydou Doumbia (Roma) - alikosa
James Horsfield (Man City) - alifunga
Seydou Keita (Roma) - alikosa
0 comments:
Post a Comment