Mashabiki wa Leeds United na Eintracht Frankfurt wamepigana nchini Austria baada ya mechi ya kirafiki ya maandalizi ya msimu mpya.
Watu 20 wameshatiwa mbaroni na wawili wanatibiwa kufuatia mashabiki wa timu zote kupigana mara baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa mjini Eugendorf.
Kwa mujibu wa Yorkshire Evening Post, mashabiki wanaokaribia 100 wa Frankfurt waliingia uwanjani kupigana na kundi la mashabiki wa Leeds.
Frankfurt walishinda magoli 2-1.
0 comments:
Post a Comment