Straika huyo raia wa Colombia amejiunga na Atletico kwa dau la Euro milioni 35 kutokea klabu ya Porto ambayo aliifungia magoli 92 katika kipindi cha miaka mitatu aliyodumu hapo.
Akitarajiwa kufuata nyayo za washambuliaji wakali waliowahi kukipiga Atletico, Radamel Falcao na Diego Coast, Martinez aliulizwa kama anaweza kuvaa viatu vyao na akajibu:
"Falcao ni Falcao, Jackson ni Jackson. Wote walifanya kazi yao na mimi nipo hapa kujaribu kufanya kazi yangu".
Pia amesifu mafanikio ya klabu yake mpya.
"Kama huijui Atletico, hujui kuhusu mpira. nadhani ni timu iliyofanikiwa kwa mengi miaka ya karibuni na inahitaji kukua zaidi.
Tazama namna Martinez alivyowasili mji mkuu wa Hispania, Madrid:
0 comments:
Post a Comment