Mabingwa wa ligi kuu England, Chelsea wamechapwa 4-2 na New York Red Bulls katika mechi ya kwanza ya maandalizi ya msimu iliyopigwa leo asubuhi nchini Marekani.
Loic Remy ndiye aliifungia Chelsea goli la kuongoza kipindi cha kwanza kabla ta wenyeji kusawazisha kupitia kwa Franklin Castellanos na kufunga goli la pili kupitia kwa Tyler Adams.
Sean Davis akafunga magoli mawili, huku goli la pili la Chelsea likifungwa na Eden Hazard.
Chelsea wanajiandaa kuchezaa na PSG Jumamosi ya wiki hii na baada ya hapo wachuana na Barcelona.
Tazama Highlights za mechi hiyo:
0 comments:
Post a Comment