Kama Cristiano Ronaldo hataki kocha wake, Rafa Benitez amchezeshe kama mshambuliaji wa kati, basi anaweza kujikuta inakula kwake kwasababu leo ameonesha uwezo mzuri dhidi ya Manchester City.
Ingawa alianza mechi kwa kushambulia kutokea kushoto, Real Madrid ikishinda 4-1 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Man City, Ronaldo alikuwa anaingia katikati na kucheza vizuri kama mshambuliaji wa kati na kufunga goli zuri.
Mshindi huyo wa Ballon D'Or alikimbia vizuri kupitia katikati akiuwahi mpira uliopigwa na Toni Kroos kabla ya kumfunga golikipa wa Man City Joe Hart.
Tazama goli la Ronaldo:
0 comments:
Post a Comment