Wednesday, July 22, 2015

Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal kwa mara nyingine tena ameahidi usajili ambao ameuita kama ni wa ‘kushtukiza’ katika kipindi hiki cha majira ya joto lakini amesisitiza kuwa kamwe hatakuwa mshambuliaji.
Van Gaal amesema hayo baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya San Jose Earthquakes, ambapo United wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 huku magoli yakifungwa na Juan Mata, Memphis Depay na Andreas Pereirra
Madachi huyo awali aliahidi kuongeza makali katika safu ya ushambuliaji kwa kumleta mchezaji ambaye hajawahi hata kuzungumziwa, lakini kwa sasa amesema hana mpango tena wa kusajili mshambuliaji.
 “Nimesoma tu kwenye magazeti kwamba nitafanya ‘surprise’ ya kusajili mshambuliaji”, alisema. Hiyo sio sawa kabisa. Itakuwa ni kitu kingine tena”.
Van Gaal aliongeza kuwa kuna machaguo mbalimbali katika nafasi ya ushambuliaji na kusema: “Tuna Rooney, anaweza kucheza kama mshambuliaji, na vyombo vya habari karibu vyote viliandika kuwa anapaswa kucheza pale, sasa nimewasikiliza na nitamchezesha pale,halafu mnaanza kuhiuliza tena maswali, sasa sijui mnataka nini ninyi.
Vilevile Javier Hernandez na pengine labda Wilson na mwingine ambaye bado sijamjua. Ni mchakato. Sina hofu yoyote juu ya nafasi ile.
Kuhusu mchezaji huyo Van Gaal amesema, “dili lipo katika mchakato. Sio mshambuliaji kama ambavyo vyiombo vya habari vimekuwa vikiripoti, Ninyi subirini tu mtaona”.
Taarifa zilizopo ni kwamba mshambuliaji wa Barcelona Pedro Rodriguez ndio yuko kwenye rada za Man United kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza nafasi tofauti uwanjani

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video