Saturday, July 11, 2015

Louis Van Gaal akifafanua baadhi ya mambo kwenye mkutano maalumu na waandishi wa habari wakati wa utambulisho wa nyota mpya Memphis Depay
Na Ramadhani ngoda.
Kocha wa Manchester United, Mdachi Louis Van Gaal amethibitisha taarifa za usajili wa mlinnzi wa Kiitaliano kutoka Torino, Matteo Darmian anayetarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya tayari kuitumikia United katika msimu ujao wa ligi na michuano mingine ya ndani na kimataifa ambayo United inashiriki.

Darmian anakwenda kuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Van Gaal katika majira haya ya joto baada ya kunaswa kwa winga wa Kidachi, Memphis Depay na tayari Muitaliano huyo amekubali kusaini kandarasi ya miaka 4 na mashetani hao wekundu wa jiji la Manchester.

Darmian anasajiliwa United kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 13 na Luis Van Gaal ameliweka wazi hilo katika mkutano maalumu na waandishi wa habari wakati wa kumtambulisha winga raia mwenzake wa Uholanzi, Memphis Depay.

“Nimezisoma hizo taarifa (za kusajiliwa kwa Darmian) kwenye vyombo vya habari. Lakini ni kweli (anakuja United),” alithibitisha Van Gaal.

Katika hatua nyingine, kocha huyo anayeelekea kwenye msimu wake wa pili tangu avae viatu vya Mskochi David Moyes, amekataa kupigia mstari taarifa za kuondoka kwa Mdachi mwenzake Robin Van Persie katika klabu hiyo na kusema kuwa taarifa yoyote kuhusu hilo itatolewa na klabu ifikapo wakati mujarrab.

“Tutakapohisi anaondoka, mtasikia kutoka Manchester United. Hatuna hizo hisia kwa sasa,” alifafanua kocha huyo juu ya taarifa za kusepa kwa Van Persie.

Van Gaal alikwenda mbali Zaidi na kuizungumzia safu yake ya ushambuliaji na malengo aliyonayo juu ya maboresho yake na kusema kuwa timu haitakurupuka kusajili mshambuliaji kwa sasa mpaka pale itakapoonekana na timu kuwa ni muhimu.

“Tuna washambuliaji wa kutosha kwa sasa. Manchester United haisajili tu,” alinena Van Gaal.

“Mimi sio mwalimu nnayetaka kusajili tu wachezaji wakati wote, nataka kuendeleza wachezaji ila wakati mwingine inatubidi kusajili,” aliongeza.

“Unaposajili ni lazima unachokisajili kiwe bora Zaidi ya ulichonacho. Lkini hilo litaonekana msimu utakapoanza kama ni kweli tunachokidhani juu ya wachezaji,” alisisitiza.

Luis Van gaal hakusita kuzungumzia hali ya mlinda mlango wa United anayehusishwa na kuhamia Real Madrid, David De gea na kusifu mwenendo wake katika kipindi chote cha maandalizi ya msimu mpya.

“Ni mchezaji wa kulipwa. Na ameonesha mwenendo mzuri sana mpaka sasa,”


“Ni kipindi kigumu kwa kocha yoyote yule. Mchezaji anapotaka kuondoka, wewe hutaki aondoke nab ado unatakiwa ununue wachezaji-ni kipindi kigumu mno,” alieleza meneja huyo juu ya sakata la golikipa wake ambaye yupo na timu akiendelea na maandalizi ya msimu mpya.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video