Washika bunduki wa jiji la London, klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza, imepata pigo mara baada ya ripoti kutoka Ureno zikieleza kuumia kwa kiungo William Calvalho.
William Calvalho mwenye miaka 23 hivi sasa, amekua akiwindwa kwa muda mrefu na timu zinazoshiriki ligi kuu nchini Uingereza, huku Arsenal wakiwa kipaumbele kumsaini kiungo huyo.
Taarifa kutoka katika klabu yake ya Sporting Lisbon, ya nchini Ureno, zinasema mchezaji huyo aliumia katika fainali za michuano ya ulaya chini ya umri wa miaka 23 mwezi uliopita nchini Israel.
Kupitia ukurasa wa Facebook wa Sporting, klabu imeandika kwa masikitiko makubwa kumkosa mchezaji huyo kwa mechi za maandalizi ya msimu pamoja na mechi za awali za ligi.
Hata hivyo baada ya kuumia katika fainali hizo za Euro U-21, Calvalho hakuonekana kuwa linaweza kuwa tatizo kubwa lakini wikiendi hii alijitonesha majeraha yake katika maandalizi ya pre-season.
William Calvalho anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha kati ya wiki 10-12 miezi mitatu.
Taarifa hizo zitakuwa zimeharibu mipango ya klabu za Uingereza kumsaka mchezaji huyo.
0 comments:
Post a Comment