kikosi cha Marekani kilichoshiriki mashindani ya kwanza ya kombe la dunia 1930 nchini Uruguay na kushinda mchezo wa kwanza dhidi ya Ubelgiji. |
Na Ramadhani Ngoda.
Wakati soka likiwa na
mengi ya kukumbuka. Leo ikiwa ni Julai 13 mwaka 2015, yapo mengi yalipata
kujiri tarehe kama ya leo miaka kadhaa iliyopita.
Julai 13 mwaka 1930,
ilikuwa ni siku ambayo kwa mara ya kwanza mashindano ya kombe la Dunia yalikuwa yanafunguliwa nchini Uruguay kwa michezo miwili ambapo timu ya taifa ya Ufaransa iliiadhibu Mexico mabao 4-1 huku Marekani wakiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya
Ubelgiji katika michezo hiyo ya ufunguzi iliyopigwa mji mkuu wa Uruguay,
Montevideo.
Fainali hizo ziliisha
kwa wenyeji Uruguay kuibuka machampioni kwa kuifunga Argentina 4-2 katika
mchezo wa fainali ambao ulikuwa ni kama marudio ya mchezo wa fainali ya Olympic
ya mwaka 1928.
aliyewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Italia (2006-2008), Roberto Donadoni |
Ukiachana na hilo,
tarehe kama ya leo mwaka 2006, ni siku ambayo Italia walimtangaza rasmi kiungo
wa zamani wa AC Milan, Roberto Donadoni anayekumbukwa kwa
kushinda mataji 6 ya Italia akiwa na Milan pamoja na mataji 3 ya Ulaya kama
kocha mkuu wa timu ya taifa hilo akichukua pahala palipoachwa na Marcelo Lippi
aliyeamua kusepa baada ya kuiwezesha Italia Kutwaa kombe la dunia katika
fainali zilizofanyika mwaka huo nchini Ujerumani mwaka huo.
kutoka kulia (Antonio Valencia, Sir Alex Ferguson, Michael Owen na Gabriel Obertan) baada ya kukamilisha usajili wao Man Utd Julai 13 mwaka 2009. |
Mashabiki wa
Manchester United watakuwa wanaikumbuka sana siku hii kwani mnamo siku kama ya
leo mwaka 2009, Sir Alex Ferguson alikamilisha usajili wa nyota watatu kwa mpigo
ambao ni Gabriel Antoine Obertan, Michael James Owen na Luis Antonio Valencia. Wachezaji ambao
walikuwa na mchango mkubwa kila mmoja kwa nafasi yake na kuiwezesha United
kutwaa ubingwa wa Uingereza msimu wa 2010/11 baada ya kuupoteza kwa Chelsea
msimu wa 2009/10. Antonio Valencia ndiye mchezaji pekee aliyedumu hadi sasa
katika kikosi cha mashetani hao wekundu baada ya wenzake wawili (Owen na
Obertan) kuuzwa.
Bastian Schweinsteiger akiwa na kombe la Dunia baada ya kushinda taji hilo na Ujerumani Julai 13 mwaka 2014. |
Kingine cha
kufurahisha ni kuwa mnamo tarehe kama ya leo (Julai 13) lakini mwaka 2014, kiungo
wa kimataifa wa Ujerumani Bastian Schweinsteiger alishinda taji la kombe la
Dunia akiwa na Ujerumani wakiifunga Argentina katika mchezo wa fainali kwa goli
pekee la kiungo aliyekuwa akikipiga naye Bayern, Mario Gotze.
Kizuri ni kuwa hii ni Siku ambayo bado inazidi kuwa na maana kubwa kwake katika maisha yake ya soka kwani tarehe kama hiyo mwaka 2015 amekamilisha usajili wake rasmi kuelekea Manchester United akimaliza kipindi chake cha kuwatumikia ‘Mabavaria’ Bayern Munich.
Kizuri ni kuwa hii ni Siku ambayo bado inazidi kuwa na maana kubwa kwake katika maisha yake ya soka kwani tarehe kama hiyo mwaka 2015 amekamilisha usajili wake rasmi kuelekea Manchester United akimaliza kipindi chake cha kuwatumikia ‘Mabavaria’ Bayern Munich.
Bastian Schweinsteiger (kulia) akiwa na Louis Van Gaal zama za utawala wake Bayern Munich. |
Kwa kuwa tunathamini kumbukumbu, Haya ni machache kati ya mengi yanayohusu soka unayoweza kukumbuka yaliojiri tarehe kama ya leo lakini miaka kadha iliyopita.
0 comments:
Post a Comment