MABINGWA wa kandanda Tanzania
bara, Young Africans leo majira ya saa 10:00 jioni wanahitaji ushindi mzuri dhidi ya KMKM ya Zanzibar ili
kujihakikishia kucheza hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Kagame linaloendelea
kutimua vumbi jijini Dar es salaam.
Wakati huo huo, KMKM nao
wanahitaji ushindi ili kujihakikishia kwenda Robo Fainali.
KMKM na Yanga SC zote zina pointi tatu baada
ya kila timu kushinda mechi moja hadi sasa, dhidi ya wapinzani mmoja, Telecom
ya Djbout.
KMKM walishapoteza mechi mbili baada ya kufungwa 2-1 na
Khartoum N na 3-1 dhidi ya Gor Mahia,
wakati Yanga SC imepoteza mechi moja tu dhidi ya mabingwa mara tano wa michuano
hiyo Gor Mahia.
Endapo KMKM
itafungwa leo, watatupa nje ya michuano
hiyo.
Yanga SC ikicheza leo itabakiwa na kibarua kigumu dhidi ya
vinara wa kundi A, Khartoum National
Club ya Sudan ambayo itakuwa ya mwisho
baada ya kucheza na KMKM .
Khartoum ina pointi sita, mabao saba ya kufunga na moja la
kufungwa, wakati Gor Mahia walio nafasi ya pili wana ponti sita, mabao matano
ya kufunga na mawili ya kufungwa.
Yanga SC
inashika nafasi ya tatu kwa pointi zake tatu, mabao manne ya kufunga na mawili
ya kufungwa, wakati KMKM ina pointi tatu, mabao matatu ya kufunga na matano ya
kufungwa.
Telecom ya
Djibouti ambayo itacheza mechi ya mwisho na Gor Mahia kabla ya kurejea kwao
imepoteza mechi zote tatu.
Ilifungwa 1-0
na KMKM, ikafungwa 5-0 na Khartoum na jana imefungwa 3-0 na Yanga SC.
Timu tatu kati ya tano za
kundi hilo zitakwenda Robo Fainali kuungana na washindi wawili wa kila kundi B
na C pamoja na mshindi wa tatu bora kutoka makundi hayo.
0 comments:
Post a Comment