Na Ramadhani Ngoda.
Wapenzi wa masumbwi
ukimwenguni wanasubiri kwa hamu burudani nyingine ya mchezo huo baada ya kambi
za mabondia Tyson Fury kutoka Uingereza na Wladmil Klitscko kutoka Ukraine
kufikia makubaliano ya kupanda ulingoni ifikapo Oktoba mwaka huu.
Pambano hilo lilikuwa
shakani kufanyika lakini baadaye mazungumzo yaliofanyika katika ofisi za chama
cha soka ulimwenguni (WBA) Mjini Panama, yalikwenda vyema na hatimaye kufikia
makubaliano na kisha kusaini mkataba kwa ajili ya pambano hilo linalotarajiwa
kufanyika mjini Dusseldorf katika ardhi ya Ujerumani.
Klitschko anayeshikilia
mataji 3 ya IBF, WBO na WBA kwa sasa, ametakiwa kutetea mataji yake dhidi ya
Tyson Fury aliyepania kuteka nyoyo za wapenzi wa ndondi ulimwenguni siku ya
pambano hilo.
Fury (26) hakusita
kutamba kuelekea pambano hilo baada ya kuandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa
twita kuwa anakwenda kuwa bondia bora duniani katika uzito wa juu.
“Mfame anayekuja
katika pambano hili kama mpiganaji bora wa uzito wa juu katika sayari hii,”
alitamba Fury dhidi ya Klitschko.
Tambo hizo bado
hazifanyi pambano hilo kuwa jepesi kwa mzawa huyo wa jiji la Manchester, kwani
Klitschko hajapoteza pambano lolote (unbeaten) tangu mwaka 2004 ikiwa ni miaka 11
sasa jambo linaloongeza ladha ya pambano hilo.
Klitschko ambaye
tarehe 5 Oktoba mwaka 2014 alimtwanga Mbulgaria aliyekuwa hajaonja kipigo
kabla, Kubrat Pulev na kutwa ubingwa wa IBF, atapanda ulingoni dhidi ya Fury
ambaye pambano lake la mwisho alilopanda ulingoni tarehe 28 Februari mwaka huu
alimtwanga Christian Hummer.
Kutokana na wengi kuwa
na shaka juu ya Fury kufanya kama alivyofanya David Haye aliyewahi kupangiwa
kuzipiga naye na Haye kujitoa kwenye pambano na baadaye kustaafu kutokana na
majeraha, Fury ameahidi kutofanya jambo kama hilo kwa lengo la kulinda heshima
aliyonayo kwa wana masumbwi.
“Naahidi sitofanya
kama David Haye. Nitampiga kwa KO (knock out) na wala msiwe na shaka juu ya hilo,”
aliandika Fury kwenye ukurasa wake wa twita.
0 comments:
Post a Comment