Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Mwesigwa Selestine ametuma salamu za rambi rambi kwa famili aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela kufuatia kufiwa na baba yake mzazi jana mjini Irinnga na mazishi yakitarajiwa kufanyika kesho mjini Iringa.
Aidha TFF imetuma salam za rambi rambi kwa kocha mkuu wa timu ya Mbeya City, Juma Mwambusi kufutia kufiwa na mama yake mzazi mjini Mbeya.
TFF pia imetuma salam za rambi rambi kwa familia ya mtangazi maarufu wa wa michezo nchini Ezekiel Malongo aliyefariki dunia jana.
Katika salam zake kwa familia ya Mwakalebela, Mwambusi na Malongo, Mwesigwa amesema wanawapa sana pole wafiwa kwa kuondokewa na wapendwa wao na kusema kwa niaba ya TFF, familia ya mpira na watanzania wote wapo nao pamoja katika kipindi hichi cha maombolezo.
0 comments:
Post a Comment