Liverpool bado wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa Christian Benteke, 24, lakini hawataki kulipa pauni milioni 32, licha ya kumuuza Sterling kwa pauni milioni 49 kwenda Manchester City (Daily Mirror), Manchester United wapo tayari kumuuza winga Angel Di Maria kwenda Paris St-Germain kwa pauni milioni 42.8 (Le Parisien), lakini United wanamtaka Edinson Cavani katika mkataba wa kumuuza Di Maria (Daily Express), Manchester City na Liverpool zinamtaka mshambuliaji wa Fulham Patrick Roberts 18 (The Sun), Chelsea wana uhakika wa kuwazidi kete Arsenal na Liverpool katika kumsajili Pedro, 27 kutoka Barcelona (Daily Star), beki wa Valencia Nicolas Otamendi, 27, yuko tayari kugoma kucheza ili kushinikiza kuhamia Manchester United (The Sun), Arsenal wametoa dau la pauni milioni 10 kumtaka beki wa Napoli Faouzi Ghoulam, 24 (Mediaset), mshambuliaji wa Arsenal kutoka Costa Rica Joel Campbell, 23, huenda akaondoka moja kwa moja huku Real Sociedad wakimtaka (Daily Mirror), Southampton wanakaribia kuziba pengo la Morgan Schneiderlin aliyekwenda Man Utd kwa kumsajili Jordy Claise kutoka Feyenoord (Daily Mail), Chelsea na Tottenham huenda wakalazimika kulipa zaidi ya pauni milioni 15 kwa mwaka ili kuutumia uwanja wa Wembley wakati wakikarabati viwanja vyao (Times), wakala wa Robert Lewandowski wamewaambia Manchester United kuwa watalazimika kulipa zaidi ya pauni milioni 35 kumsajili mshambuliaji huyo wa Bayern Munich (Independent), meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ametupilia mbali tetesi kuwa Mesut Ozil anaondoka Emirates (Sky Sports), Manchester United wanazungumza na kipa kutoka Argentina Sergio Romero anayesakwa pia na Roma. Kipa huyo ni mchezaji huru baada ya kuondoka Sampdoria (Sky Sport Italia), West Ham wanajiandaa kutoa pauni milioni 5 kumnunua mshambuliaji wa Manchester United Javier Hernandez 'Chicharito' (The Sun), Roma wapo tayari kuongeza dau lao hadi pauni milioni 25 kumnunua Edin Dzeko kutoka Manchester City (Sky Sport Italia).
Wednesday, July 15, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment