Baadhi ya mashabiki wa Arsenal bado wana hamu ya kuona klabu yao inasajili mchezaji mkubwa majira haya ya kiangazi.
Leo zimetoka tetesi kwamba, nyota wa Bayern Munich, David Alaba anaweza kutua Emirates.
Alba mwenye miaka 23 ni injini ya Bayern, anaweza kucheza kama kiungo au Mlinzi.
Kutokana na umuhimu wake katika klabu ya Bayern, inaonekana tetesi ya kutua Arsenal ni ndoto ya mchana.
Tetesi ya Alba kutua Arsenal imeanzaje?
Mtumiaji wa Twitter@arsenalbarclays, mwenye wafuasi 14,000 ameeneza umbea huo akisema kwamba amesoma stori hiyo kwenye gazeti la jana la beIN Sports .
Upupu huo umesambaa mithiri ya moto uliowashwa nyikani!
Hapa chini ni baadhi ya Tweets juu ya stori ya Alba kutua Arsenal;
0 comments:
Post a Comment