Ukurasa wa mbele wa gazeti la Hispania la Mundo Deportivo leo umeandika stori ya usajili ikiihusisha klabu ya Arsenal.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, Arsene Wenger anataka kumsajili kiungo wa ulinzi wa Barcelona, Sergi Samper mwenye umri wa miaka 20.
Taarifa hiyo inadai kwamba Arsenal wanajiandaa kutuma ofa ya kumsajili chipukizi huyo wa Barcelona B ambapo wanataka kutoa dau la Euro milioni 12.
Mundo Deportivo linasema kwamba Arsenal walijaribu kumsajili Samper ili awe mrithi asilia wa Mikel Arteta, lakini jitihada zao ziigonga mwamba.
Video ya Sergi Samper hii hapa chini;
0 comments:
Post a Comment