Friday, July 24, 2015


 Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania wenye umri chini ya miaka 20 (Tanzanite) tayari ipo Zambia kwa  ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Young She-Polopolo. 
Tanzanite inayowania kufuzu kwa Fainali za Kombe Duniwa mwaka 2016 nchini Papua New Guinea, itacheza mchezo huo wa marudano kesho Jumamosi, jijini Lusaka. 
Katika mchezo wa awali uliofanyika takribani wiki mbili zilizopita, Tanzanite ilipoteza mchezo wake nyumbani baada ya kufungwa kwa mabao 4 – 0, hivyo kuhitaji kushinda zaidi ya mabao 5 – 0 ili kuweza kusonga katika hatua inayofuata.
Msafara wa Tanzanite umeongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Blassy Kiondo utajumuisha makocha Rogasian Kaijage (kocha mkuu), Edna Lema (kocha msaidizi), Peter Manyika (kocha wa makipa), Christina Luambano (Daktari), Mwanahamis Abdallah (mtunza vifaa) na Meneja Furaha Francis.
Wachezaji waliopo Zambia ni Stumai Abdallah, Shelder Boniface, Donisia Minja, Najiat Abbas, Neema Kiniga, Happyness Mwaipaja, Jane Lucas, Anastazia Katunzi, Anna Mwaisura, Janet Pangamwene, Gelwa Rugomba, Blandina Ambros, Amina Ramadhan, Asha Shaban, Maimuna Hamis, Zuwena Hamis, Amisa Athuman na Wema Richard.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video