Mshambuliaji mpya wa Coastal Union aliyesajiliwa majira haya ya kiangazi kutokea, Stand United, Mnigeria, Abasarim Chidiebele amesema atawatumia wagosi wa kaya kama daraja la kutua klabu kubwa za Simba, Yanga au Azam FC.
Chidiebele aliyefunga magoli 11 msimu uliopita amesema kuwa ndoto zake ni kucheza timu za kiwango cha juu Tanzania.
"Mimi kazi yangu mpira, nimecheza Stand msimu uliopita, msimu ujao nitaichezea Coastal Union". Amesema Chidiebele: "Coastal ni timu kubwa, lakini kwa Tanzania Simba, Yanga na Azam ndio timu kubwa zaidi. Nitatumia nafasi hii kuzichezea baada ya msimu ujao, nitajituma na mwishoni mwa msimu ujao nitakuwa mfungaji bora".
0 comments:
Post a Comment