West Brom imekamilisha uhamisho wa Rickie Lambert kutokea Liverpool kwa ada ya paundi milioni 3.
Baada ya kufuzu vipimo leo, Lambert amesaini mkataba wa miaka miwili.
Straika huyo mwenye miaka 36 ambaye msimu uliopita aliifungia Liverpool magoli 3 katika mechi 36, pia alikuwa akihusishwa kutua Leicester na Tottenham, lakini timu ya Tony Pulis imefanikiwa kunasa saini yake.
Baada ya kutangazwa rasmi na West Brom, imefahamika kwamba Lambert amejumuishwa katika kikosi kinachocheza usiku huu na timu yake ya zamani ya Bristol Rovers kujiandaa na msimu mpya.
0 comments:
Post a Comment