Moja ya stori inayotembea sana kwa sasa ni Cristiano Ronaldo kuhusishwa kurejea Manchester United, lakini kocha mkuu wa klau hiyo, Louis van Gaal amekanusha taarifa hizo.
Mreno huyo alidumu miaka sita Man United chini ya Sir Alex Ferguson kabla ya kuhamia Real Madrid kwa dau la paundi milioni 80 mwaka 2009.
Van Gaal amesema Unted inahitaji mshambuliaji mmoja, lakini sio Cristiano Ronaldo.
Ronaldo anahusishwa kurudi Old Trafford kwasababu hana mahusiano mazuri na kocha wa sasa wa Madrid,Rafa Benitez.
Van Gaal amesema:
"Barcelona ina (Lionel) Messi, Neymar na (Luis) Suarez. Tunahitaji kupata aina hii ya wachezaji".
Mashabiki wa United wangefurahi kuona kipenzi chao Ronado anarejea, lakini Mholanzi huyo aliongeza "Hiyo haiwezekani kwasababu una klabu, inategemea unataka kutumia kiasi gani".
Hii inamaanisha Van Gaal anahofia bei ya kumchukua Ronaldo.
0 comments:
Post a Comment